MSONDO, SIKINDE PRESHA JUU MPAMBANO WAO MEI 20


Wakati ikielezwa kuwa maandalizi yote yamekamilika juu ya mpambano wa Sikinde na Msondo Jumamosi hii, bendi hizo presha ziko juu huku kila moja ikifanya siri kubwa kwenye mipango  yao.

Mratibu wa onyesho hilo Abdulfareed Hussein ameimbia Saluti5 kuwa kila kinachohitajika kwenye maandilizi ya mpambano huo kipo mkao wa kula kuanzia jukwaa kubwa, vyombo vya kisasa hadi nakshi mbali mbali.

Msondo na Sikinde wataumana ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni ikiwa ni mara yao ya kwanza kufanya onyesho la pamoja ndani ya kiwanja hicho.

Viongozi wa bendi zote mbili wameahidi kuwa patachimbika siku hiyo.

No comments