MSUVA AGOMBANIWA NA KLABU TATU NCHINI MISRI

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva neema kubwa imemuangukia baada ya klabu tatu za Misri kugombea saini yake lakini kila moja ikiweka kiasi cha sh mil 150 mezani endapo klabu  yake ya Yanga itakubaliana na kila kitu.

Taarifa zinasema tayari moja ya klabu nchini Misri ya Al Ettihad imeshatua Jangwani kuomba ridhaa ya klabu hiyo kuingia katika meza ya mazungumzo ya kumaliza usajili huo haraka.

Alizungumza na saluti5, Msuva alisema tayari anajua kila kitu kuhusu ofa hizo tatu lakini sasa anasubiri maamuzi ya klabu yake kwa kuwa bado yuko katika mkataba wa kuitumukia yanga unaomalizika mwakani.

Msuva alisema katika ofa hizo tatu, Al Ettihad iliyopo katika nafasi ya nne katika Ligi ya Misri ndio wanaongoza katika kuifukuzia saini yake ambapo amewaomba viongozi wa klabu yake kutanguliza maslahi na kipaji chake katika kurahisisha uhamisho huo.

"Ni kweli kuna hizo ofa tatu kutoka huko Misri, ni faraja kwangu kuona katika juhudi zangu kitu kama hiki kikija ili niweze kupiga hatua zaidi mbele na hizi ni habari njema kwa Yanga na nchi yangu”, alisema Msuva.


No comments