MSUVA ASISITIZA "YANGA TUTAHAKIKISHA TUNABEBA UBINGWA ILI KUMFARIJI MANJI WETU"

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Yanga, Simon Msuva amesema kuwa watahakikisha wanafanya kila waliwezalo kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ili kumfariji mwenyekiti wao Yusuf Manji ambaye alipatwa na matatizo binafsi.

Winga huyo ambaye ni kinara wa mabao katika kikosi cha George Lwandamina alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha wanamfanya mwenyekiti wao kuwa na furaha wakjati wote.
“Lazima tupambane mpaka mwisho wa mchezo lakini lengo hasa ni kubeba ubingwa najua hiyo itakuwa faraja kwake baada ya kupata matatizo binafsi” alisema Msuva.

“Sisi ni binadamu tunajua hali mwenyekiti aliyopitia tangu apatwe na matatizo Binafsi nadhani kama wachezaji tunatakiwa kusimama katika sehemu yetu ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu bara ili iwekama njia ya kumfaliji” aliongeza Simon.


Yanga ipo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu bara kwani katika mchezo iliyobaki watalazimika kucheza ugenini mechi moja tu dhidi ya Mbao FC ambayo ni Ngeni kwenye michuano hii baada ya kupanda daraja msimu uliopita.

No comments