MSUVA: USHINDI HUU NI MAALUM KWA YUSSUF MANJI


Baada ya Yanga kuifunga Prisons ya Mbeya 2-0 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, winga Simon Msuva amesema ushindi huo  ni maalum kwa mwenyekiti wao Yussuf Manji.

Akiongea baada ya mchezo huo, Msuva akasema: “Ushindi huu uwe zawadi kwa mwenyekiti wetu Manji, tunajua alikuwa na matatizo na hatuna namna nyingine ya kumpa furaha zaidi ya njia hii ya ushindi.

“Tunashukuru makocha wetu waliusoma mchezo na kufanya mabadiliko yaliyozaa matunda, lakini kubwa zaidi hii ni zawadi kwa mwenyekiti wetu”.

Mabao ya Yanga yalifungwa na  Amissi Joselyn Tambwe na Obrey Chirwa.

No comments