MUHOGO MCHUNGU AWATAKA WATANZANIA WASIENDELEE KUOMBOLEZA VIFO VYA WANAFUNZI WA LUCKY VICENT

MWIGIZAJI Abdallah Mkumbila “Muhogo Mchungu” ameshauri Watanzania kuacha kuendelea kuomboleza msiba wa wanafunzi na walimu wa shule ya Lucky Vicent kwa madai kwamba kuendelea kufanya hivyo ni kuzidi kuwatia majonzi wafiwa.

Akiongea na saluti5, Muhogo Mchungu amesema kuwa, kwa kawaida msiba unapotokea una muda wake wa kuomboleza ambao si zaidi ya siku tatu kwa watu ambao si ndugu wa karibu, hivyo maombolezo ya ziada hivi sasa yanapaswa kuachwa kwa walengwa wenyewe.


“Kuendelea kuomboleza ni kuzidi kuwakumbusha wafiwa tukio ambalo sasa wanapaswa kuanza kulisahau na kurudi kwenye shughuli zao nyingine kwasababu maisha mengine bado yanaendelea hata baada ya janga hilo.”

No comments