Habari

MUUMIN, CHOCKY, NYOSHI KUPAMBANISHWA ESCAPE ONE …ni El Clasico ya magwiji wa dansi

on

Waimbaji magwiji wa dansi Ally Chocky, Mwinjuma Muumin na Nyoshi el Saadat watapambanishwa kwenye jukwaa moja Mei 19 jijini Dar es Salaam.
Onyesho hilo lililopewa jina la ‘Magwiji El Clasico’ limepangwa kufanyika ndani ya ukumbi wa Escape One, Mikocheni ambapo kila mmoja atapigiwa na ‘live band’.
Mratibu wa onyesho hilo Dj Elly wa Clouds FM, ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo limeandaliwa ili kumaliza ubishi miongoni mwa waimbaji hao ambao kila mmoja anatamba kuwa ndiye mfalme wa dansi la kisasa lililofanyiwa mageuzi makubwa mwishoni mwa miaka ya 90.
Dj Elly amesema onyesho hilo litasindikizwa na Khadija Kopa, Msagasumu, MC Soud na Madada 6 huku kiingilio kikitajwa kuwa ni sh. 15,000 na 25,000 kwa V.I.P.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *