MVUA: MASHAUZI CLASSIC YAAHIRISHA ONYESHO LA MANGO GARDEN LEO USIKU


Mvua zinazoendelea kunyesha mfululizo jijini Dar es Salaam zimeendelea kuwa kikwazo kwa maonyesho mengi ya muziki.

Kundi la Mashauzi Classic ambalo hupiga Mango Garden kila Alhamisi, limeahirisha onyesho lao la leo usiku kutokana na mvua inayendelea kunyesha tangu asubuhi.

Hii inakuwa ni Alhamisi ya tatu mfululizo kwa Mashauzi Classic kushindwa kupiga Mango kutokana na mvua.

Mkurugenzi wa Mashauzi Classic Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa kwa hali ilivyo leo hawana namna nyingine zaidi ya kuahirisha onyesho.

“Mvua haina dalili ya kukata, hakuna haja ya kuwapa shida wasanii na mashabiki wetu, wacha tuangalie wiki ijayo mambo yatakavyokuwa,” amesema Isha.

No comments