MVUA YAVUNJA SHOW YA EL CLASICO KABLA CHOCKY NA NYOSHI HAWAJAPANDA …Muumin pekee ndo ‘kijogoo’.


Saa 7 na dakika 35 Muumin anamaliza ngwe yake, kisha linapanda kundi la Madada Sita ambalo linatumbuiza hadi saa 7:56, wasanii wa Nyoshi wanapanda jukwaani, lakini kabla hawajafanya lolote inashuka mvua kubwa.

Wakati Muumin anamaliza ngwe yake alisema: “Waimbaji wa ukweli tumemaliza, sasa tunawapisha wauza sura”, akimaanisha Nyoshi na Chocky.

Mvua inakuwa kubwa kiasi cha kuvunja show, jukwaa halina turubai wala ukumbi hauna paa. Watu wanaguna kwa mzaha Muuuuumin!!! Wakimaanisha kaleta mvua.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa, show saa 8 kamili za usiku inavunjika kabla ya Nyoshi na Ally Chocky hawajapanda jukwaani. Mpangilio mbovu wa ratiba ulioje!!

Show hiyo iliyoitwa El Classico ambayo ilikuwa inafanyika Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam, ilihusisha mpambano wa Muumin, Chocky na Nyoshi.

No comments