MWALIKO WA SIMBA BUNGENI WAMPA HAJI MANARA JEURI YA "KUCHONGA"

MWALIKO walioupata Simba bungeni Dodoma juzi umempa kiburi aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara kutamba kuwa klabu yake ni “chama kubwa” katika soka hapa Bongo.

 “Simba ni kubwa nchi nzima, bara la Afrika na duniani. Tuna wabunge, mawaziri na hadi marais na waheshimiwa wengine ambao ni wanachama wa klabu hii na mwaliko wetu bungeni ni uthibitisho tosha,” amesema Manara mwenye maneno mengi ya shombo.

“Tuna wanachama pale bungeni, waheshimiwa ambao ni wafurukutwa wa Simba ambao walitualika twende kukalionyeshe Kombe letu pale bungeni kama mojawapo ya shamrashamra ya kusherehekea ushindi huu.”


“Tulihitaji sana Kombe hili na pia tulihitaji mno nafasi hii kwa ajili ya kwanza kuleta heshima kwa klabu na zaidi ni kupata uwakilishi wa kucheza michuano ya kimataifa ambayo mara yetu ya mwisho kushiriki ilikuwa ni mwaka 2012 na sasa Simba inarudi kwenye nafasi yake,” alitamba.

No comments