MWANAFALSAFA ASEMA BIFU ZA KIJINGA ZINAHARIBU MUZIKI BONGO

MSANII bongofleva, Mwanafalsafa amesema kuwa muziki wa Bongo unafanywa kienyeji sana na umekosa ubunifu kutokana na bifu zisizokuwa na maana.

Nyota huyo alisema kuwa hakuna kampuni za maana zinazoweza kufanya kazi kwa weledi  na kusukuma gurudumu la sanaa hapa nchini.

"Niliwahi kuwa na wazo la kufanya muziki kupitia lebo lakini  sioni ni kwa vipi naweza kupiga hatua kwasababu nafahamu mambo mengi yanafamywa kienyeji,” alisema rapa huyo.


“Hakuna lebo makini inayoweza kumtoa msanii toka chini na kumpandisha kwenye daraja la juu, hapa kila kitu kinafanyika kwa mazoea pasipokuwa na ubunifu,” aliongeza.

No comments