MWASITI AAHIDI MAMBO MAKUBWA... kuachia kazi mpya mwezi ujao

MSANII  mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Mwasiti Almas amedai huu ni wakati wake wa kushirikiana vizuri na uongozi wake mpya ili kuhakikisha anafanya mambo makubwa katika muziki wake.

Mwimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo "Kaa Nao" amesema kuwa muda mchache aliokaa na uongozi wake mpya amegundua anaweza kufanya mambo makubwa katika muziki wake tofauti na zamani.

“Kwanza nashukuru Mungu project yetu ya kwanza imeanza vizuri, nimepokea komenti nyingi nzuri imenifanya nione ni dalili nzuri katika muziki wangu pamoja na management yangu mpya,” alisema Mwasiti.


Aliongeza “Kwahiyo muda huu kwetu ni kazi ya juu ya kazi no majungu. Pia tunajipanga kuachia kazi mpya mwezi Juni. Kaa Nao tayari umeshafanya vizuri sana. Sina mengi zaidi ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano waliotuonyesha, sitawaangusha huu ni muda wetu wa kazi tu.”

No comments