MWENENDO WA LIGI KUU BARA WAMDUWAZA KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA

ALIYEKUWA kocha wa Simba, Dyler Kerr raia wa Uingereza amesema kuwa anashangazwa na mwenendo wa Ligi Kuu Tanzania bara huku maoni ya wadau wa michezo yakionekana kuipa Yanga nafasi kubwa ya kubeba ubingwa huo kwa mara nyingine.

Kocha huyo amesema kwamba amekuwa akifuatilia kwa makini kila hatua ambayo inapigwa na klabu yake tangu aondoke lakini anasikitika kuona maoni yanaegemea katika kuipa Yanga ubingwa kwa mara nyingine tena.

“Najua kila hatua inayopigwa huko Simba, ni timu yangu lakini sielewi kwanini watu wamepoteza imani kiasi cha kutoipa nafasi ya kubeba ubingwa kuliko Yanga,” alisema kocha huyo.

“Nafikiri walianza vizuri mwanzoni kabla ya mambo kugeuka ghafla ndio maana watu wamekosa imani nao,” aliongeza kocha huyo.


Kocha huyo alifukuzwa Simba baada ya kuwa na mwendelezo wa matokeo mabovu ambapo alikubali kipigo cha mabao 2-0 kwenye mchezo wa watani wa jadi uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

No comments