MWIMBAJI WA WASHAWASHA CLASSIC ACHENGUA SHOO YA MASHAUZI CLASSIC MANGO GARDEN JANA

MWIMBAJI mahiri wa kiume wa Washawasha Classic Min Band, Omary Sosha usiku wa jana alijikuta akiulipua ukumbi wa Mango Garden kwa makofi ya furaha, baada ya kupanda jukwaani na kupagawisha mashabiki kwa wimbo wa zamani uitwao “Mazoea Yana Taabu”.

Ilikuwa kwenye milango ya saa 7:30 hivi usiku, ndipo MC wa Mashauzi Classic waliokuwa wakitumbuiza ukumbini hapo, alimwomba Sosha kupanda jukwaani ili kusalimia kisanii, ndipo mkali huyo alipopata fursa ya kuwakosha mashabiki kwa dakika chache.

Kilichoonekana kuwapagawisha zaidi mashabiki ni namna mwimbaji huyo alivyokuwa akiuimba kwa nakshi wimbo huo na baadae kuwapa kionjo cha wimbo “Je, Utanipenda” wa msanii wa bongofleva, Diamond Platnumz.

Mbali ya Omary Sosha, msanii mwingine aliyekaribishwa jukwaani kutoa “ladha” alikuwa ni Iqujaan Iqbar ambaye ni bosi wa bendi ya Kongamoyo ya jijini Dar es Salaam.

No comments