MWINJUMA MUUMIN AIMBA "KILIO CHA YATIMA" JUKWAANI KUOMBOLEZA KIFO CHA DOGO MFAUME

KATIKA shoo yao ya “Magwiji El Clasico” iliyopigwa jana Ijumaa ndani ya Escape One, Mikocheni Dar es Salaam, mwimbaji Mwinjuma Muumin alimaliza ngwe yake jukwaani kwa kibao “Kilio cha Yatima” ambacho alisema ni maalum kwa ajili ya msiba wa Dogo Mfaume.

Dogo Mfaume aliyefariki Jumatano na kuzikwa jana Ijumaa majira ya saa saba mchana, alikuwa msanii wa miondoko ya mchiriku na enzi za uhai wake alitamba sana na vibao vya “Heleni” na “Kazi ya Dukani”.

“Namalizia na kibao Kilio cha Yatima, ambacho ni maalum kwa ajili ya misiba mizito miwili iliyolikumba taifa, mmoja ni wa wale wanafunzi kule Karatu na mwingine ni wa msanii mwenzetu Dogo Mfaume,” alisema Muumin.

Hata hivyo, shoo ya jana ilishindwa kumalizika baada ya mvua kubwa kukung’uta ghafla na waandaaji kuamua kuivunja huku magwiji wengine ambao ni Ally Chocky na Nyoshi el Saadat wakiwa bado hawajapanda jukwaani.    

No comments