MWISHO WA KUTHIBITISHA MASHINDANO YA MSTAHIKI MEYA NI MEI 15

CHAMA cha ngumi za riadha mkoa wa Dar es Salaam (DABA)kimetaja tarehe ya mwisho ya uthibitisho kuskushiriki wa mashindano ya Mastahiki wa jijini Dar es Salaam ambapo kamati ya usibitisho ni Mei 15, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na katibu mkuu wa chama hicho Wamboi Mangore alipozungumza na saluti5 jijini Dar es Salaam.

Alisema mashindano hayo yatashirikisha klabu na timu za majiji mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania, hivyo lengo la kutaja siku ya mwisho ni kutaka mashindano hayo yaandaliwe kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa.

“Tunatarajia majiji tulioyapa mialiko kwa siku zijazo yatathibitisha kuwepo kwa ushindani mkubwa kwa mwaka huu kutokana na milango bado ipo wazi,”alisema Mangole.

Katibu huyo alisema kuwa mbali na kutoa mialiko hiyo kwa majiji ya nje mkoa Dar es salaam pia wilaya tano zilizopo katika jiji la Dar es Salaam pamoja na taasisi za majeshi ya ulinzi na usalama pia zinatajwa kuthibitisha ushiriki wao na kufanya mashindano kuwa na msisimko na ushindani mkubwa.

Kuhusiana na mabondia wa kutoka nje ya nchi Mangore alibainisha kuwepo kwa washiriki kutoka katika jiji la Mombasa na wengine ni kutoka nchini Botswana.


Katibu mkuu huyo alizitaja zawadi za washindi kuwa ni pamoja na Kombe la Medali ambapo mashindano yanatarajia kuanza Mei 23 hadi 29 mwaka huu katika uwanja wa ndani wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam.

No comments