NEW AUDIO: ISIKILIZE "SHIKA MOYO" NYIMBO MPYA YA IVORY BAND
Wimbo mpya wa Ivory Band “Shika Moyo” umeachiwa rasmi na bila kusita Saluti5 inakuwekea hapa uusikilize.

Ngoma hiyo ambayo imerekodiwa katika studio za Amoroso, ni utunzi wake Rama Pentagon. 

Kama tulivyoleza hapo awali, kupitia wimbo huu, Ivory Band wamejivua kabisa kwenye koti la muziki wa rumba na ule masebene makali unaopigwa na bendi nyingi za Kitanzania na badala yake wamekuja na muundo wa kipeke yao.

Ni wimbo uliojaa utulivu, ujumbe mzuri wa mapenzi na mpangilio bak kubwa wa vyombo. Kaa mkao wa kula kuisubiri nyimbo hii kali. ISIKILIZE HAPO JUU

No comments