NEW AUDIO: TOT WAMLILIA MPIGA SOLO WAO MIRAGE KUPITIA WIMBO "KALALE PEMA" ...mazishi yake ni kesho mchana Dar es SalaamTOT Band imepakua wimbo mpya wa kumlilia mpiga solo wa wao Mirage Halitopo (pichani juu) aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Wimbo unakwenda kwa jina la “Kalale Pema Mirage”.

Huyu anakuwa msanii wa pili wa TOT kufariki ndani ya miezi miwili. Wa kwanza alikuwa ni mpiga bass Samwel Mshana aliyefariki Aprili 8 ambaye alikuwa swahiba mkubwa wa Mirage na walikuwa wakiishi nyumba moja.

Hata piki piki iliyotajwa kuwa chanzo cha kwanza cha Mshana kuugua na hatimaye kufariki ilikuwa ni ya Mirage.

Ndani ya wimbo huu, TOT wanaimba kuwa ni siku 40 tangu Mshana atutoke, Miraji nenda umetimiza ahadi.

Mazishi ya Mirage (Miraji) ambaye ni raia wa Congo (DRC) yatafanyika kesho (Jumamosi) mchana katika makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa, jijini Dar es Salaam. Msiba uko Mwananyamala nyuma ya ukumbi wa CCM Mwinjuma.

No comments