NEYMAR AKINUKISHA BARCELONA, AKOROMEANA NA KOCHA MSAIDIZI


Supastaa wa Barcelona, Neymar ameripotiwa kukoromeana na kocha msaidizi wa timu hiyo Juan Carlos Unzue.

Hali hiyo ilitokea mazoezini baada ya kocha huyo msaidizi kumwambia Neymar awekeze zaidi akili yake kwenye soka lake.

Wakati Unzue anayetarajiwa kurithi mikoba ya Luis Enrique akiongea na Neymar na kumpa mbinu za kimichezo, ndipo hali ilipochafuka kwa wawili hao.
No comments