NGOMA ASEMA "NIMEWACHOMOLEA SIMBA, NIMEWAAMBIA SIWEZI KUCHEZEA TIMU NYINGINE ZAIDA YA YANGA BONGO"

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Donald Ngoma amevunja ukimya akitamka kwamba kamwe hawezi kuvaa jezi nyekundu na kuitumikia Simba hapa nchini na kama akiamua kubaki basi ni kusaini Yanga.

Akizungumza na saluti5, Ngoma amesema Simba walionyesha nia ya kuhitaji huduma yake lakini amewaambia wazi kwamba hataweza kucheza timu nyingine zaidi ya Yanga ambayo ndiyo iliyomleta nchini akitokea FC Platinumz ya Zimbabwe.

Ngoma alisema hatma yake ya kubaki nchini itajulikana hivi karibuni atakapoingia katika meza ya mazugumzo ya kuongeza mkataba na uongozi wa Yanga na kwamba hana kinyongo chochote katika kubaki katika klabu hiyo.

Alisema, endapo atashindwa kukubaliana na Yanga atarudi nchini kwao Zimbabwe kujiunga na kikosi chake cha zamani cha Platinumz ambao bado wanamuhitaji arudi katika timu hiyo.


“Siwezi kukataa, Simba walinihitaji lakini niliwaambia sina mpango wa kucheza timu yoyote tofauti na Yanga hapa Tanzania, nafurahi kuona wameonyesha nia ya kunihitaji lakini kwa sasa msimamo wangu ndiyo huo,” alisema Ngoma.

No comments