NI MIUJIZA TU ITAKAYOINYIMA CHELSEA UBINGWA ...yaishusha daraja Middlesbrough kwa kichapo cha 3-0


Tony Pulis, kocha wa West Bromwich Albion, ambayo itaikaribisha Chelsea Ijumaa ijayo, alikuwepo Stamford Bridge kuangalia Middlesbrough ikishushwa daraja na vijana wa Antonio Conte

Kipo alichojifunza? Pengine kikubwa atakachokifanya ni kuichelewesha tu Chelsea kutangaza ubingwa Premier League mapema, lakini ni wazi kuwa miamba hiyo ya London haizuiliki tena.

Chelsea inahitaji pointi tatu tu katika michezo mitatu iliyobakisha huku ikicheza mechi zake mbili za mwisho kwenye uwanja wa nyumbani. Anazuilika vipi? ni miujiza pekee inayoweza kuzuia kombe kwenda darajani.

Jumatatu usiku Chelsea wameichabanga Middlesbrough 3-0 na kuwashusha daraja kwa mabao ya Diego Costa, Marcos Alonso na Nemanja Matic.

Chelsea (3-4-1-2): Courtois; Cahill, Luiz (Terry 84 mins), Azpilicueta; Moses, Fabregas, Matic, Alonso; Pedro (Chalobah 81), Hazard (Willian 72); Costa

Middlesbrough (4-1-4-1): Guzan; Fabio, Chambers, Gibson, Friend; Clayton; Traore (Bamford 57), Forshaw (Leadbitter 56), De Roon, Downing; Negredo (Gestede 82)
No comments