“NIMEPOTEZA KILA KITU, SINA BUDI KUANZA UPYA” ASEMA ROMA MKATOLIKI

RAPA ambae alijaza vichwa vya habari baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana, Roma Mkatoliki  amesema kuwa imembidi kuanza kujipanga upya  kabla ya kurudi kwenye sanaa kwa nguvu zote.

Rapa huyo amesema kuwa walipovamiwa kwenye studio za Tongwa Records walipoteza kazi zao nyingi ambazo zilikuwa zitoke hewani.

“Bado sijaweza kukaa sawa tangu tukio lile litokee, kwa kweli nimepoteza vitu vingi zikiwemo kazi zangu za sanaa hivyo nalazimika kufanya kazi mara mbili ya uwezo wangu,” alisema rapa huyo.

Roma Mkatoliki alivamiwa na kundi la watu wasiojulikana kwenye Studio za Tongwa Records zilizopo Masaki, jijini Dar es Salaam na kuibiwa baadhi ya vifaa vyao muhimu vya sanaa.

No comments