NYOTA YA FARID MUSSA YANG'ARA ZAIDI HISPANIA, ATABIRIWA MAKUBWA NA VIONGOZI WA TIMU YAKE

KIUNGO wa timu ya DC Tenerife ya nchini Hispania, Mtanzania Farid Mussa ameanza kutabiriwa makubwa baada ya kuanza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Katika mchezo dhidi ya Deportivo Tenerife, alifanikiwa kufunga mabao mawili na kutoa pasi ya bao moja kwenye ushindi wa mabao 5-1 ambao waliupata.

Baada ya mechi hiyo makocha wa Deportivo walimwambia Farid kuwa yuko mbioni kucheza kwenye Ligi kubwa baada ya kuonyesha uwezo mkubwa.

“Viongozi wa Deportivo walinifuata baada ya kufunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya goli, wakanipongeza kwa uwezo niliouonyesha,” alisema Farid.

“Walinitia moyo na kunambia sina muda mrefu nitapenya kwenye Ligi kubwa za ushindani,” aliongeza kiungo huyo aliyetokea Azam FC.


Tangu ajiunge na timu hiyo, Farid amekuwa akipangwa kucheza mechi za vijana ili kupandisha kiwango chake lakini hivi sasa mambo yameanza kumuendea vizuri baada ya kuanza kufunga mabao muhimu.

No comments