OMOTOLA JALADE WA NIGERIA ASEMA UMAMA WA NYUMBANI HAUTAMSTAAFISHA KUCHEZA MUVI

STAA wa filamu za maigizo nchini Nigeria, Omotola Jalade amesema kuwa pamoja na jukumu la malezi ya watoto alilokuwa nalo, bado hajafikiria kuachana na filamu.

“Nina familia kubwa hivi sasa lakini hainibani kufanya kazi zangu za filamu, ni suala la kuwa na mpangilio mzuri wa ratiba ya siku,” amesema Omotola.

“Ni kweli kuna ugumu wakati mwingine kwa sababu malezi ni suala muhimu zaidi lakini sishawishiki kuachana na filamu,” ameongeza.


Staa huyo mwenye mvuto wa mapenzi nchini Nigeria, ana mume na watoto watatu kwenye ndoa yake, lakini hilo halimfanyi aigeuzie kisogo filamu.

No comments