OMOTOLA JALADE WA NOLLYWOOD ASEMA HAJAWAHI KUMSALITI MUMEWE KWA KUCHEPUKA

STAA wa filamu za Nollywood, Omotola Jalade ambaye anatajwa kuwa na mvuto wa kimapenzi, anasema kuwa tangu afunge ndoa na mumewe ambaye ni rubani wa ndege, Ekeinde hajawahi kuchepuka.

“Mume wangu ananiheshimu sana, hivyo hata mimi namuheshimu sana hata kama hakuna ambaye ana muda wa kumchunga mwenzie katika mahusiano wetu,” amesema Omotola.

“Mimi ni mtu maarufu ndio maana watu wanataka kunihusisha na kila mtu ambaye anaonekana kuwa karibu kwa ajili ya kazi, ukweli ni kuwa sijawahi kuchepuka naheshimu ndoa yangu,” aliongeza dada huyo.

Omotola ambaye amepata umaarufu kupitia soko la filamu, alimalizia kwa kusema kuwa ni suala ya kisaikolojia tu kuanza kufuatiliana kila hatua ambayo mwenzio anapiga.

No comments