ORIGINAL DAR MUSICA YAJA NA BONANZA BAB KUBWA FRIENDS CORNAR MANZESE

CLUB Friends Corner, Manzese Argentina, jijini Dar es Salaam kesho inatarajiwa kuwa na bonanza bab kubwa litakalopambwa na bendi ya muziki wa dansi ya Original Dar Musica chini ya mwimbaji mahiri Jado FFU.

Taarifa kutoka ndani ya Club Friends Corner zinasema kuwa, bonanza hilo limepangwa kuanza kuunguruma majira ya saa 11:00 jioni na kuendelea hadi majogoo.

“Bonanza hili ni maalum kwa wakazi wa Manzese na vitongoji jirani, hivyo tunaomba wajitokeze kwa wingi ili kufarijisha nafsi zao kwa burudani ya kukata na shoka kutoka kwa Original Dar Musica,” imesema taarifa hiyo.

No comments