PAUL POGBA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI


Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amefiwa na baba yake mzazi Fassou Antoine Pogba (79) aliyekuwa akiugua hospitalini.
Mwezi Machi mwaka huu Pogba alimtembelea baba yake na kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa na baadae kutupia picha Instagram na kusindikiza na maandishi: "Heri ya kuzaliwa baba yangu mpendwa, najisikia fahari kuwa mtoto wako".
Baba huyo alikuwepo jukwaani kwenye mechi za Euro 2016 akimsapoti mwanae aliyekuwa akiichezea timu ya taifa ya Ufaransa ambapo katika moja ya picha zilizopigwa, ilimuonyesha akiwa na watoto wake Florentin na Mathias huku Paul Pogba akivua jezi yake baada ya mchezo na kubakiwa na fulana iliyokuwa na maandishi ya kumsifu baba yake.
 Pogba akiwa na fulana yenye maandishi ya kumsifia baba yakeBaba
 Baba yake Pogba akiwa uwanjani kumtazama mwanae
Pogba alipomtembelea baba yake hospitalini mwezi Machi mwaka huu

No comments