PICHA 10: MC SOUDY NA MSAGASUMU WALIVYOFUNGUA SHOW YA EL CLASICO NDANI YA ESCAPE ONE


Msanii wa miondoko ya ladha na singeli MC Soudy ndiye aliyepata bahati ya kufungua onyesho kubwa la muziki wa dansi lililopewa jina la El Clasico linalofanyika usiku huu ndani ya Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

El Classico ni mpambano wa magwiji watatu wa dansi Ally Chocky, Mwinjuma Muumin na Nyoshi el Sadaat.


MC Soudy akapiga show ya kutaka na kuonyesha uwezo wa hali ya juu wa kucheza na njia za uimbaji na baada ya hapo akafuata mkali mwingine wa uswazi Msagasumu ambaye makali yake yanaeleweka.

Baada ya MC Soudy na Msagasumu, sasa amepanda Mwinyuma Muumin na kundi lake.
MC Soudy jukwaani
 Wasanii wa Muumin walipokuwa wakifuatilia show ya MC Soudy
 Wasanii wa Muumin
 Wasanii wa Nyoshi wakifuatilia onyesho
 MC Pilau akiongoza show nzima ya El Clasico kwa umakini wa hali ya juu
 Msagasumu jukwaani
 Msagasumu
 MC Soudy
MC Soudy akilimiliki jukwaa
Mdau Hamis Slim akifualia show


No comments