PICHA 10: MWINJUMA MUUMIN AJIFUA HADI USIKU MNENE KUJIWEKA SAWA NA "MAGWIJI EL CLASICO" LEO

MKALI wa sauti ya kulalamika kwenye muziki wa dansi, Mwinjuma Muumin jana alimalizia kujifua kwa staili ya aina yake akijiandaa na pambano la leo la “Magwiji El Clasico” litakalorindima baadae ndani ya Escape One, Dar es Salaam.

Saluti5 ilitembelea kambi ya mazoezi ya Mwinjuma Muumin ndani ya Equator Grill na kushuhudia namna Muumin alivyokuwa katika mazoezi makali yaliyoanzia mchana hadi usiku, huku akionekana kutoridhika na hatua aliyofikia kwenye mazoezi hayo.

Hata hivyo, Muumin amejinasibu kuwagaragaza Ally Chocky na Nyosh el Saadat anaotarajiwa kuvaana nao leo, akisema kuwa ana silaha nzito za maangamizi, anazoamini zitawatoa jasho kisawasawa wapinzani wake hao kwenye pambano hilo litakalopambwa na Khadija Kopa, MC Sudi, Madada Sita na Msaga Sumu.


“Sina wasiwasi kwani niko vizuri sana kama unavyoona, nawaomba mashabiki wangu tu waje kwa wingi Escape One kushuhudia namna ninavyowatoa nishai Chocky na Nyosh,” amesema Muumin.   

HAPA CHINI NI PICHA 10 ZA NAMNA MWINJUMA MUUMIN ALIVYOFUNGA RASMI MAZOEZI YAKE JANA
 Wanenguaji wa Mwinjuma Muumin wakiwa kwenye mazoezi makali ya staili za kucheza
 Mcharazaji gitaa la solo akiweka vyema nyuzi kwa ajili ya pambano la leo
 Mpapasa kinanda Yusuph Teggo nae akipasha
 Mpiga Tumba akikoleza ngoma zake
 Mwimbaji Abuu Muhumba akiitikia moja ya nyimbo walizokuwa wakifanyia mazoezi
 Mkung'utaji gitaa la Bass akiwajibika
 Hamza Salleh "Waninga" kwenye Drums
 Muumin akilalamika
Mkali wa gitaa la Rhythm akifanya yake

No comments