PICHA 14: SIKINDE ILIVYOIPIGA 2-1 MSONDO TRAVERTINE …mvua yavunja show muda wa serikali


Jana usiku bendi mbili kongwe Msondo Ngoma na Sikinde ziliumana vizuri katika ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Umati mkubwa ukafurika ndani ya ukumbi huo kushuhudia mpambano wa Msondo na Sikinde. Dansi likamimininwa vilivyo, watu wakambumbwa na mzuka wa kucheza, ikawa raha ndani ndani ya burudani.

Kila bendi ikatakiwa kutumbuiza kwa dakika 60 jukwani kabla ya kupisha bendi nyingine ambapo mpangilio ungendelea hivyo hadi mwisho wa onyesho.

Ratiba ya show hiyo ambayo haikuwa na msanii wala bendi nyingine ya kusindikiza, ikaanza saa 3 kamili kwa Sikinde kuwa wa kwanza kuburudisha kabla ya Msondo kupanda jukwaani saa 4 kamili na kuungurumisha dansi lao hadi saa 5 kamili.

MC wa onyesho hilo Masoud Masoud akatambulisha wasanii wa Msondo kabla ya kuirejesha tena Sikinde saa 5 na robo ambao walitumbiza kwa kiasi cha kama dakika 40 hivi kabla mvua kubwa haijashuka na kupelekea onyesho kuvunjika saa 6 kamili, muda halali wa serikali wa kumaliza maonyesho kwenye kumbi za wazi.

Sikinde wakawa wametumbuiza mara mbili, Msondo mara moja na hapo ndipo 2-1 ya Sikinde inapokuja – kwamba angalau mashabiki wao wamewaona mara mbili.


Kinyume na mvua, burudani ilikuwa nzuri na kama ilivyo ada ya bendi hizi, ilikuwa ngumu kubaishiri ni bendi ipi itaibuka mbabe.

Kwa kawaida makali na silaha zote za bendi hizi huonekana kwenye raundi mbili za mwisho, lakini hadi mvua inavunja onyesho bado hazina ya zana za maangamizi ya mpambano wa Sikinde na Msondo, ilikuwa haijafichuliwa.
 Bitchuka wa Sikinde akifanya yake
 Habib Jeff wa Sikinde akizicharaza drums
 Kalama Regesu wa Sikinde akiimba moja ya nyimbo za Sikinde
 Wazee wa Msondo ...Said Kibiriti (kushoto) na Abdulfareed Hussein 
 Zahoro Bangwe wa Msondo (kushoto) akiteta na Bitchuka wa Sikinde muda mfupi kabla ya onyesho
 Mabela wa Msondo akipiga solo gitaa
 Mashabiki kwa raha zao
Baadhi ya waimbaji wa Sikinde jukwaani
 MC wa onyesho Masoud Masoud (kulia) akimkaribisha jukwaani mchambuzi gwiji wa muziki wa dansi Rajab Zomboko
 Zomboko akiwa na mdau wa dansi Chiki Mchoma
 Mjusi Shemboza wa Sikinde
 Wazee wazima wakisakata dansi
 Shaaban Dede wa Msondo akiimba kwa hisia
Waimbaji wa Msondo jukwaani


No comments