PICHA 25: TWANGA PEPETA MANGO WEE WACHA TU … siku zote ingekuwa hivi tungekuwa tunaongea mengine


Usiku wa kuamkia leo, The African Stars “Twanga Pepeta” ilipiga show iliyojaa vitu adimu na kuwapa siku njema mashabiki wa muziki wa dansi.

Ama kwa hakika kama Twanga Pepeta wangekuwa wanapiga show zao za kila wiki kwa mpangilio huu, basi kile kilio cha kushuka kwa muziki wa dansi kisingekuwepo kwa bendi hii.

Mpangilio wa nyimbo (playlist), ulikidhi mahitaji, waimbaji wakautendea haki muda - hakukuwa na blah blah jukwaani, wapiga vyombo wakaonyesha utundu wa kupiga nyimbo nyingi kwa mfumo wa ‘non stop’.

Kwa ujumla uwajibikaji na nidhamu ya jukwaa ilikuwa ya hali ya juu huku ‘sound’ ikiwa ya kuridhisha kiasi cha kutosha.

Baada ya nyimbo za kunakili, program rasmi ya nyimbo za Twanga ikaanza kwa wimbo mpya “Yananitesa” maarufu kama “Prison Love” utunzi wake Khalid Chokoraa, kufungua pazia.

Zilipigwa nyimbo 11 za Twanga Pepeta ambapo mpangilio ulikuwa kama hivi:
Saa 4:40 – “Prison Love”
Saa 5:00 – “Kumekucha”
Saa 5:21 – “Shamba la Twanga”
Saa 6:08 – “Uso Chini”
Saa 6:30 – “Dunia Daraja”
Saa  6:53 – “Prison Love” kwa mara ya pili.
Nyimbo zote hizi zilipigwa kwa mfumo wa ‘non stop’

Saa 7:20 Kiongozi wa bendi Luizer Mbutu akatoa matangazo machache ya ratiba ya wiki ya bendi.

Saa  7:23 – “Kuolewa”
Saa 7:41 – “Rafiki Adui”

Saa 8:10 utambulisho wa mameneja wapya Martin Sospeter na Zonte Mahundu.

Saa 8:16 – “Mtu Makini”
Saa 8:28 – “Mwana Dar es Salaam”
Saa 8:57 – “Mkiwa Hadeki”

Saa 9:08 onyesho likafikia tamati.


Pata picha 25 za onyesho hilo la Twanga Pepeta ndani ya Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Haji BSS
 Mtangazaji wa zamani wa Radio One na ITV Isack Gamba akiwa na Komandoo Hamza Kalala
 James Kibosho kwenye drums
 Jojoo Jumanne na bass lake
 Kalala Jr na Khalid Chokoraa walisisimua pale walipowavua mawigi madansa wa kike na kutinga kichwani
 Khalid Chokoraa alipendeza sana
 Kirikuu naye akizigonga drums
 Chipukizi mpya wa Twanga Pepeta Joshua akifanya yake
 Kushoto ni mwimbaji chipukizi wa kike wa Twanga Fetty akiimba sambamba na Luizer Mbutu
 Muonekano kamili wa Fetty na Luizer
 Kutoka kushoto ni Jojoo Jumanne, Miraji Shakashia na God Kanuti
 Mameneja wapya wakitambulishwa ...Martin Sospeter (kushoto) na Zonte Mahundu (kulia)
 Rapa aliyerejeshwa kundini, Mirinda Nyeusi akishusha mistari yake
 Msanii mlemavu akisalimia jukwaa la Twanga
 Shabiki wa kutupwa wa Twanga Fredito Mopao akitoa bakshishi
 Fredito Mopao akimtunza mihela mpiga bass Hosea
 Rapa chipukizi wa Twanga Teophil
 Makamuzi yanaendelea
 Watu wakiwajibika jukwaani
 Meneja wa Mashauzi Classic Sumaragar na mkurugenzi wa Wakali Wao Thabit Abdul
 Kanuti, Hosea na Thabit Abdul kwenye magitaa
 Chokoraa akiteta na Dj Elly wa Clouds FM
 Isack Gamba ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa Radio Koloni ya Ujerumani akionyesha kuvutiwa na show ya Twanga
 Victor Nkambi kwenye kinanda
Kutoka kushoto ni Hajj BSS, Luizer Mbutu, Mirinda Nyeusi na Kalala Jr

No comments