PICHA 5: SEMSEKWA AREJEA SKY MELODIES YA DODOMA …aibuka na rap ya “Weka Mambo”


Rap mwenye ‘madini’ mengi Grayson Semsekwa, amerejea tena bendi ya Sky Meledies ya Dodoma.

Ijumaa usiku Semsekwa alishiriki ipasavyo onyesho la bendi hiyo lililofanyika ndani ya ukumbi wa Carnival mjini humo.

Hii ni mara ya pili kwa Semsekwa kuitumikia bendi hiyo inayoongoza na Nicco Milimo ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mwezi Machi mwaka jana kabla hajatimkia Songea.

Grayson alifanya kazi iliyotuka ndani ya bendi za Extra Bongo, African Revolution “Diko Diko” Twanga Chipopopo na Twanga Pepeta.

Rapa huyu pia ni mtunzi mzuri na moja ya nyimbo zake zilizobamba sana “Regina” ya Extra na “Shamba la Twanga” ya Twanga Pepeta.

Katika onyesho la Sky Melodies Ijumaa usiku ndani ya Carnival, Semsakwa akatamba na rap yake mpya “Weka Mambo” ambayo ilisisimua ukumbi mzima.
 Semsekwa akikamua na Sky Melodies mjini Dodoma Ijumaa usiku
 Semsekwa akifanya yake ndani ya ukumbi wa Carnival, Dodoma Ijumaa usiku
 Moja ya 'maua' ya Sky Melodies ...hatari!!!
 Drumer boy wa Sky Melodies 
Nicco Milimo rais wa Sky Melodies


No comments