POGBA AMZUNGUMZIA RASHFORD NA FREE-KICK YAKE YA MAAJABU


Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amempongeza 'mkombozi' wao  Marcus Rashford — na kufichua kuwa mshambuliaji huyo alijua kuwa atafunga  free-kick yake.         

United ilikuwa inaelekea kupata sare tasa kwenye mechi ya Europa League dhidi ya   Celta Vigo Alhamisi usiku, kabla Rashford hajaokoa jahazi. 

Pogba anasema Rashford alimwambia kuwa anadumbikiza mpira wavuni. 

"Wakati anakwenda kupiga free-kick ile aliniambia anakwenda kufunga na kweli akafanya hivyo"No comments