POGBA ASEMA MAN UNITED BADO INA KAZI NZITO KWA CELTA VIGO


Manchester United bado ina kazi kubwa ya kutinga fainali ya Europa League licha ya kuongoza  1-0 dhidi ya Celta Vigo. Hayo yamesemwa na kiungo wa timu hiyo, Paul Pogba.


Timu hizo zinarudiana Alhamisi ijayo ndani ya Old Trafford ambapo watu wengi wameanza kuamini kuwa United tayari imenusa fainali.

Pogba anasema: "Bado hatujafanya chochote, bado hatujacheza dakika 90 zingine na tunakabiliana na timu nzuri.

"Tunapaswa kuwaheshimu kwa sababu ni mara ya kwanza wanacheza nusu fainali ya Ulaya katika historia yao na watakwenda kutoa upinzani mkali Old Trafford".
No comments