RAMSEY NOAH ASEMA FANI YA FILAMU NI "MTIHANI" KWA WAIGIZAJI WENYE NDOA ZAO

STAA wa filamu nchini Nigeria, Ramsey Noah amesema kuwa ni kweli wakati mwingine fani ya maigizo inawaweka kwenye wakati mgumu na wale ambao wanahusiana nao kimapenzi.

Ramsey amesema kwamba kuna baadhi ya maeneo unapopewa kuigiza yanaweza kuleta shida kidogo kwenye ndoa.

“Ni kazi inayohitaji moyo, kuna wakati unalazimika kumuacha ndani mkeo na kwenda kuigiza usiku wa manane tena sehemu za mapenzi,” alisema nyota huyo.

“Tunaishi tu kwavile tumezoea na ndio kazi yetu, lakini inaumiza kidogo na hasa mnapokuwa bado wachanga kwenye mahusiano,” aliongeza.

Ramsey ni mmoja kati ya mastaa wanaoripotiwa kuwa na mvuto wa kimapenzi nchini Nigeria ambapo filamu iliyomtangaza ni “My Love” aliyocheza kama mtoto wa masikini aliyeangukia kwenye penzi la mtoto tajiri.

No comments