RAMSEY NOAH SASA KUIBUA VIPAJI VYA WASANII CHIPUKIZI

RAMSEY Noah ambaye ni staa wa filamu nchini Nigeria amesema kwamba yuko mbioni kuanzisha mradi wa kuibua vipaji vya wasanii wachanga kwenye fani ya maigizo.

“Itakuwa ni sehemu ya kulipa fadhila kwa mashabiki wangu kwa kuanza na mradi wa kuibua vijana wenye vipaji vya uigizaji,” amesema.

“Hata mimi nilikuwa msanii mchanga, kama nisingeungwa mkono na watu nadhani nisingekuwa hapa,” ameongeza.


Ramsey amejipatia umaarufu kupitia filamu ya “My Love” ambayo iliiteka soko la kimataifa na kuuza nakala nyingi zaidi.

No comments