RAPA YUNG6IX ASEMA BADO "YUPOYUPO" SANA TU... adai hana mpango wa ndoa kwa sasa zaidi ya kusaka hela

RAPA Yung6ix amesema kuwa hana mpango wa suala linaloitwa ndoa kwa hivi sasa zaidi ya kuwaza kutafuta pesa ili atimize ndoto ya kuwa bilionea.

Staa huyo alibainisha kwamba hayupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamke yeyote pamoja na umaarufu wake kupitia muziki.

“Kila mtu ana kipaumbele chake kwenye maisha suala la mahusiano ya kimapenzi halisumbui akili yangu kikubwa na waza kutafuta fedha kwa nguvu ili niwe bilionea” alisema rapa huyo.

“Nimeshawahi kuwa na mahusiano huko nyuma lakini kwasasa hapana sina mtu ninaehusiana nae” aliongeza.


Yung6ix alikazia kwa kusema kuwa wakati mwingine suala la kuwa kwenye uhusiano rinaludisha nyuma harakati zakusaka maendeleo.

No comments