RASHFORD AKUMBUSHIA ENZI ZA RONALDO MANCHESTER IKICHUNGULIA FAINALI YA EUROPA LEAGUE


Marcus Rashford anafunga kwa free-kick tamu dakika ya 67 na kuipa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya Celta Vigo.

Ushindi huo wa uliopatikana uwanja wa ugenini kwenye nusu fainali ya Europa League, unaiweka United katika nafasi nzuri ya kutinga fainali ambapo sare ya aina yoyote ndani ya Old Trafford itatosha.

Aina ya free-kick aliyopiga Rashford imeadimika sana Manchester United tangu kuondoka kwa Cristiano Ronaldo aliyekuwa ‘mchawi’ wa mipira iliyokufa Old Trafford.

Kiungo Paul Pogba akaonyesha thamani yake kwa kutawala dimba la kati na kutoa pasi za mwisho ambazo kama washambuliaji wa United wangezitumia vizuri, basi kikosi cha Mourinho kingeondoka na ushindi mzito.

CELTA VIGO (4-2-3-1): Alvarez 7.5, Hugo Mallo 6 (Beauvue 90+2 mins), Cabral 6, Roncaglia 6, Jonny 6, Wass 7 (Jozabed 74), Radoja 7, Hernandez 6, Aspas 6, Sisto 6.5, Guidetti 7


MANCHESTER UNITED (4-1-4-1): Romero 6, Valencia 7, Bailly 6, Blind 7.5, Darmian 6, Herrera 6, Fellaini 6.5, Lingard 6, Pogba 8, Mkhitaryan 6 (Young 78, Smalling 89), Rashford 7.5 (Martial 80)

No comments