REHEMA TAJIRI AKUMBUSHIA ALIVYOFUMANIWA NA KUPIGWA CHUMA KICHWANI NA MKE WA MAX BUSHOKE

REHEMA Tajiri amekumbushia namna alivyoshonwa nyuzi tatu kichwani baada ya kupigwa na chuma na mke wa mpenzi wake wa zamani mwanamuziki mkongwe, Max Bushoke, aliyemtaja kwa jina la “mama Lutha”.

Amesema sababu ya hayo yote ni namna alivyotokea kumpenda kupita kiasi Bushoke ambaye wakati huo alikuwa akiitumikia bendi ya Mlimani Park Sikinde.

“Unajua mimi kihistoria nikipenda huwa napenda haswaa na wakati mwingine napagawa kiasi cha kuonekana kama sina akili nzuri vile na kadri ninavyokaa na mpenzi ndio ninavyozidi kupagawa kwake,” amesema.

Akikumbushia zaidi tukio hilo la kupigwa vna chuma na mama Lutha, Rehema amesema kuwa uhusiano wao wa siri ulimfikia mke wa Bushoke ambaye alianza kuwawinda nae kutokana na kupagawa kimahaba hakuwa anajali.

“Siku moja Bushoke alinichukua hadi kwa kaka yake kutembea wakati kumbe mkewe alikuwa akitufuatilia na alipotukuta ndipo kasheshe lilipoanza na kunipiga na chuma kichwani,” amesema Rehema.


Amesema tukio hilo ilimfanya apasuke na kuvujwa na damu nyingi ambapo kwa taharuki alitoka mbio hadi nyumbani kwa aliyekuwa mpuliza Domo la Bata wa Sikinde, Yussuf Benard ambaye alimsaidia kumpeleka hospitali na hata hivyo asubuhi yake Bushoke alimfuata kwao na mahaba yakaendelea kama kawaida.

No comments