RIO FERDINAND NA MICHAEL OWEN WASEMA RASHFORD NI ZAIDI YA IBRAHIMOVIC


Mastaa wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand  na Michael Owen wanaamini kuwa Marcus Rashford ni zaidi ya Zlatan Ibrahimovic.
Kinda huyo aliifungia United bao pekee kwenye mchezo wa Europa League dhidi ya Celta Vigo kwa free-kick bab kubwa.
“Kuwa na Zlatan kwenye timu na kufunga zaidi ya magoli 20 ni jambo jema," alisema Ferdinand kuptia  BT Sport.
"Lakini linapokuja suala la uchezaji na kuhaha uwanja mzima, kupambana huku muda wote ukiwafungisha tela mabeki, Zlatan hayupo katika umri unaomruhusu kufaya hivyo.
"Huyu dogo (Rashford). Anakupa kitu cha ziada, wachezaji wa viungo ni lazima wafurahie kucheza nae."

Michael Owen alikubaliana na tathmini ya Ferdinand juu ya washambuliaji  wa United kwa kusema: "Nadhani wachezaji wenzie wangependa kucheza na Rashford kwa sababu anakupa vitu vya zaida".

No comments