ROMARIO ACHEKELEA MSONDO NGOMA KURUDI MIKONONI MWA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI

MPULIZA Saxophone nguli na rapa wa Msondo Ngoma Music Band, Roman Mng’ande “Romario” amesema amefarijika kwa bendi hiyo kurudi chini ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA).

Romario amesema kuwa, anamini hivi sasa mambo yatakuwa safi zaidi ukilinganisha na wakati walipokuwa wakijitegemea kutokana na kwamba watakuwa na usimamizi mzuri wa bendi.

Amesema kuwa, uzuri zaidi kwa sasa unakuja hasa kwa vile wanakuwa kwenye chama, huku wakiwa na uhakika wa kulipwa (mishahara) hata inapotokea wasipofanya kazi kwa muda mrefu.

“Kujitegemea kuna uzuri na ubaya wake ndugu yangu, unajua ilipofikia ilikuwa hatuna tena wadhamini kwa hiyo kujitegemea ikawa ni shughuli pevu na tukawa tunaishi maisha ya kubahatisha tu,” amesema Romario.


“Tuna haki ya kufurahi hivi sasa kwani maisha yamekuwa mazuri mara 80 kwani bendi imeshasajiriwa kila kitu na kama unavyoona, tumeanza kupewa magari na mambo mengine makubwa mazuri yanakuja.”

No comments