RYAN GIGGS AMPA USHAURI ‘NASAHA’ MOURINHO


Nyota wa zamani wa Manchester United RYAN GIGGS anaamini Jose Mourinho atahitaji kufanya harakati kubwa za usajili dirisha la kiangazi.

Giggs anasema kocha huyo wa United atahitaji kusajili wachezaji wanne au watano kama kweli anataka kupigania taji la Premier League msimu ujao.
Manchester United ilitumia pauni milioni 150 kiangazi kilichopita kwa usajili wa Paul Pogba, Eric Bailly, Henrikh Mkhitaryan na Zlatan Ibrahimovic.
Michael Carrick anaelekea kupewa mkataba mpya huku Ibrahimovic anatarajiwa kurejea dimbani mwaka 2018 baada ya kupona goti.
Hatma ya Wayne Rooney iko mashakani baada ya kupoteza namba kwenye kikosi kinachoanza.
Giggs anaamini wachezaji wote hao wanatakiwa kutafutiwa mbadala. "Nafasi ya Michael Carrick inahitaji mchezaji mpya,” anasema Giggs.
"Ibrahimovic atakuwa nje mwaka mzima. Nadhani anahitajika mshambuliaji mpya. Sina uhakika na kitakachotokea kwa Rooney, lakini kwa uhakika Mourinho anahitaji wachezaji wapya wanne au watano”.

No comments