SEIF MAGARI, BIN KLEB WAANZA MAKEKE YANGA SC

VIGOGO wanaojua fitna ya soka; Abdallah Bin Kleb na swahiba wake Seif Ahmeid wamefanya maamuzi mazito ya kuhakikisha klabu yao ya Yanga inatwaa taji la ubingwa, baada ya kuingia vitani kuhakikisha taji hilo linatua Jwangwani kwa mara ya tatu mfululizo.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema vigogo hao ambao walirudi rasmi katika majukumu ya kuisaidia timu hiyo wakiitikia wito wa mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji wamejipanga kuhakikisha kwa vita yoyote, Yanga inabaki na ubingwa msimu huu.

Taarifa zinasema, baada ya Yanga kupoteza taji la FA, wawili hao wakishirikiana na wajumbe wa Kamati ya mashindano waliamua kuificha timu mjini Geita ambapo itarudi leo kuwamaliza Prisons ya Mbeya huku vigogo hao wakiisafirisha na kulipa kila kitu katika ziara hiyo.


Vigogo hao wamekubaliana kwamba katika vita hiyo ya ubingwa ni kwamba Simba haitakiwi kuisogelea Yanga kwa namna yoyote huku ushindi wa mechi zao zote tano zilizosalia zikipigiwa hesabu kali kwa kuhakikisha hakuna makosa yanayofanyika.

No comments