SEKILOJO CHAMBUA AKIMIMINIA SIFA KIKOSI CHA SERENGETI BOYS... ashauri kufanyiwa kazi safu ya ushambuliaji

MCHEZAJI wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa Stars, Sokilojo Chambua amepongeza mwenendo wa timu ya vijana ya Serenget Boys ambayo inashiriki kwenye michuano ya Afrcon nchini Gabon.

Gwiji huyo wa soka hapa nchini amesema kuwa benchi la ufundi la timu hiyo limefanya kazi kubwa ya kukisuka kikosi hicho pamoja na changamoto ndogondogo zilizopo kwenye baadhi ya maeneo.

“Serengeti Boys wana kikosi imara, wanacheza kitimu kuna na muunganiko mzuri kwenye benchi la ufundi isipokuwa kuna haja ya kufanyia kazi safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa ikipoteza nafasi nyingi za wazi kama ilivyokuwa kwenye mechi dhidi ya Angola,”alisema Chambua aliyewahi kuwika akiwa Yanga.

“Tungeweza kupata idadi kubwa ya mabao kwenye mechi dhidi ya Angola kama safu ya ushambuliaji ingekuwa makini,” aliongeza.


Ni mara ya Kwanza kwa Tanzania kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Africon tangu ilipoanzishwa ramsi mwaka 1995.

No comments