SERENGETI BOYS KUISAMBARATISHA ANGOLA LEO

BAADA ya kupata sare ya bila kufungana kwenye mchezo dhidi ya Mali, kikosi cha timu ya taifa ya vijana “Serengeti Boys” kinatarajiwa kuimaliza angola katika mechi inayopigwa leo.

Kocha wa kikosi hicho, Bakari Shime, amesema kuwa mchezo wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi, mali umesaidia kuondoa hali ya hofu kwa nyota wake.

“Tunashukuru kwa kutopoteza mchezo wetu wa kwanza na matokeo yake yalisaidia kuondoa hali ya hofu kwa wachjezaji hivyo sasa tupo kamili kwa ajili ya mchezo wa leo,” amesema kocha huyo.

“Tunaomba Watanzania wazidishe dua zao ili tuweze kuvuka hatua hii ya makundi na kupata ushindi kwenye mechi ya leo na Angola,” ameongeza.  


Kikosi cha Serengeti Boys kilichangaza watu baada ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya bingwa mtetezi, Mali ambaye anahofiwa kwenye kundi B.

No comments