SERENGETI BOYS YABADILISHIWA KITUO CHA KAMBI GABON... sasa wataweka maskani Libreville badala ya Portville

TIMU ya taifa ya vijana, Serengeti Boys ambayo imepiga kambi ya wiki moja nchini Cameroon imebadilishiwa kituo nchini Gabon ambapo mwanzoni ilifahamika kuwa wangeweka maskani katika mji wa Portville lakini sasa wamehamishiwa Libreville.

Serengeti Boys imekuwa na mwenendo mzuri kwenye mechi zake za kirafiki ambapo hivi karibuni walifanikiwa kuifunga Cameroon kwa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jijini Yaunde.

Timu hiyo ya vijana imepangwa katika Kundi B ikiwa na timu za Niger, Angola na Mali ambako watafungua nayo mchezo Mei 15, mwaka huu.

Kutokana na mabadiliko hayo, Kundi A lenye timu za Cameroon, Ghana, Guinea pamoja na  wenyeji Gabon, litakuwa mjini Port Gentil.


Ikiwa watafanikiwa kubeba ubingwa huo watakuwa wameandika historia mpya kwa soka la Tanzania ambalo lina uhaba wa makombe katika michuano yoyote inayotambuliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF). 

No comments