SERENGETI BOYS YAJIHAKIKISHIA USHINDI DHITI YA MALI LEO

BAADA ya michuano ya Kombe la AFCON kufunguliwa rasmi jana, timu ya taifa ya vijana “Serengeti Boys” leo inatarajia kushuka dimbani huku ikiwa na matarajio ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo dhidi ya Mali.

Kocha wa timu hiyo, Bakari Shime amesema kuwa kikosi chake kimekomaa kuweza kuibuka na matokeo mazuri baada ya kuweka kambi yenye ubora sambamba na michezo kadhaa ya kirafiki.

“Tunajua ubora wa Mali lakini kikosi changu kipo vizuri kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo wetu wa kwanza kwa sababu tumekaa pamoja kwenye mazingira mazuri kwa muda mrefu,” alisema Shime.

“Kikosi kina hali ya ushindi, wachezaji wote wapo vizuri na wanajua umuhimu wa kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza,” aliongeza kocha huyo.

“Tumecheza mechi nyingi za kirafiki na kupata matokeo mazuri, hivyo kilichobaki ni dua za Watanzania tuweze kuvuka mtihani huu wa kwanza.”


Serengeti Boys inatarajia kucheza leo mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mali ikiwa ni mara yake ya kwanza kwa Tanzania kupata nafasi ya kushiriki kwenye michuano hii tangu ilipozinduliwa mwaka 1995.

No comments