SERENGETI BOYS YAWAOMBA RADHI WATANZANIA KUTOLEWA AFCON

STAA wa timu ya taifa ya vijana “Serengeti Boys”, Kelvin Nashoni amewaomba msamaha Watanzania baada ya kutolewa kwenye michuano ya Afcon nchini Gabon.

Serengeti Boys ilitolewa kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa na Niger kwa bao 1-0.

“Tunajua namna tulivyowaumiza Watanzania, tunaomba radhi kwa yote yaliyotokea. Tulijaribu kupambana lakini bahati haikuwa kwetu,” alisema staa huyo walipokuwa kwenye uwanja wa ndege wa Brazaville nchini Congo wakiwa njiani kurudi Tanzania.

“Tunaomba radhi kwani halikuwa lengo letu kupoteza mchezo ule, hata sisi tukiwa kama wachezaji tumeumia sana,” aliongeza.

Serengeti Boys ilitua nchini Jumanne baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo katika hatua za makundi ambapo ilimaliza kwa jumla ya pointi 4 sawa na Niger ambayo walitofautiana kwa mabao ya kufunga.

No comments