SERIKALI YATANGAZA NEEMA KWA WANAMICHEZO... yaanzisha mchakato wa kutengeneza mabilionea

WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba serikali sasa imeanza mchakato wa kutengeneza mabilionea kutumia sekta ya michezo ili baadae waje kuisaidia nchi yao kutokana na utajiri.

Waziri mkuu amesema hayo usiku wa Ijumaa katika Holeli ya Serena, Jijini Dar es Salaam wakati wa halfa maalumu ya kuichangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys inayohudhuliwa na wadau mbalimbali akiwemo waziri wa habari utamafduni sanasa na michezo Dk Harrison Mwakyembe.

“Tumejifunza vya kutosha jinsi michezo inavyotoa mabilionea kwenye nchi mbalimbali duniani ambao wanachangia pia maendeleo ya nchi zao kwa kiasi kikubwa kwenye uchumi, hivyo nasi hatuna budi kupita njia hiyo na sasa naamini kwamba tumeanza na tunaendelea,” amesema waziri mkuu.

Zaidi ya sh. mil. 200 zimechangwa usiku huo katika hafla hiyo kwa ajili ya Serengeti Boys inayotarajiwa kushiriki fainali za U/17 Afrika nchini Gabon Mei, mwaka huu.


Na waziri mkuu akawahamasisha Watanzania kuchangia zaidi ili kutimiza lengo la upatikanaji wa sh. bil 1 zisaidie ushiriki wa timu hiyo kwenye fainali hizo zinazotarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28, mwaka huu.

No comments