SEYDON AMMIMINIA SIFA MTAYARISHAJI ALIYEMGONGEA NGOMA YA "SIO POA"

MAN 5 ni kati ya watayarishaji wa muziki wa siku nyingi, mahiri na aliyewaibua wasanii wengi, hususan wa muziki wa kizazi kipya, ila inaonekana kama vile bado hafahamiki barabara kwa wadau.

Msanii Seydon ambaye hivi karibuni amepakua ngoma yake mpya ya ‘Sio Poa’, ameibuka na kuinyanyua thamani ya produza huyo akisema kuwa amechangia kumbadilisha kwa kiasi kikubwa.

Seydon amesema kwamba, Man 5 ambaye awali alikuwa kwenye Studio ya ‘Good Music’ kabla ya hivi karibuni kuhamia ndani ya DM Records, Kigogo Luhanga, jijini Dar es Salaam, ni moto wa kuoteambali.

“Ukifanya kazi na Man 5 unakuwa na uhakika wa asilimia nyingi tu ya kutusua kwasababu ana uwezo wa kukubadilisha na kukuongezea kitu ambacho awali ulikuwa huna,” amethibitisha Seydon.

“Binafsi, mwanzoni nilikuwa mcxhanaji tu lakini hivi sasa ukisikiliza ngoma yangu ya ‘Sio Poa’ nimeimba na nimefanya vyema sana, hayo yote ni matunda ya man 5. Sina cha kumuongelea zaidi ila kiukweli jamaa yuko vizuri,” ameongeza Saydon.

No comments