SEYDON ATAJA SABABU YA KUCHELEWA KWA VIDEO YA WIMBO "SIO POA"

MKALI wa bongofleva, Said Makamba “Seydon” ametaja sababu inayofanya kuchelewa kwa video ya kibao chake kipya cha “Sio Poa” alichowashirikisha Makomando kuwa ni matatizo ya kifamilia yaliyomkumba Director wake, Fadhili Ngoma.

“Tulikuwa tumeshaanza kuchukua picha za video lakini kwa bahati mbaya Fadhili Ngoma akapatwa na msiba hivyo ikabidi tusimamishe zoezi hilo,” amesema Seydon ambaye awali alitikisa na kibao chake cha ‘Ndoto’.

“Hata hivyo, muda si mrefu tutaanza tena shughuli hiyo ya uchukuaji picha ambapo naamini itakamilika haraka na kichupa hicho nitakiachia mara tu baada ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kumalizika,” ameongeza mkali huyo.


Seydon amewataka mashabiki wake kuendelea kumvutia subira wakati huu ambapo anatayarisha video hiyo, huku akijinasibu kukonga nyoyo za wengi kutokana na kazi hiyo kuwa funika bovu.

No comments